Mamlaka ya Maji Zanzibar - ZAWA

Call Directions Website Contact the organization

Mamlaka ya Maji Zanzibar - ZAWA Mamlaka ya Maji ya Zanzibar (ZAWA) ni taasisi ya Serikali ilionzishwa chini ya Sheria. Na. 4 ya 2006

30/10/2026
ZAWA YAENDELEA NA ULAZAJI WA BOMBA LA MAJI FUMBA AFCON CITYPicha za matukio zikionyesha mafundi wa Mamlaka ya Maji Zanzi...
29/10/2026

ZAWA YAENDELEA NA ULAZAJI WA BOMBA LA MAJI FUMBA AFCON CITY

Picha za matukio zikionyesha mafundi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) wakiendelea na kazi ya ulazaji wa bomba la maji katika uwanja wa mpira unaoendelea kujengwa eneo la Fumba, Fumba Afcon City.

Kazi hiyo ni sehemu ya jitihada za kuimarisha miundombinu ya maji na kusaidia upatikanaji wa huduma za maji katika eneo hilo.

Kitengo cha Uhusiano – ZAWA
Fumba
29 OKTOBA 2026

Mafundi wa ZAWA wakiwa katika Kazi ya ulazaji wa Bomba la Maji eneo la Mwera minanasini ili kurejesha huduma ya maji saf...
28/10/2026

Mafundi wa ZAWA wakiwa katika Kazi ya ulazaji wa Bomba la Maji eneo la Mwera minanasini ili kurejesha huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa maeneo hayo.

Eneo hilo limekosa maji kutokana na bomba kupata athari ya ujenzi wa Kituo cha Dala Dala Mwera Minanasini.

Kazi hiyo inatarajiwa kukamilika kesho jioni pamoja na huduma kurejeshwa kwa wananchi.

Kitengo cha Uhusiano – ZAWA
Masingini
28 OKTOBA 2026

Tunaendelea na matengenezo ya bomba la maji Masingini linalotoa maji kutoka Matangi ya maji Masingini na kupeleka maeneo...
28/10/2026

Tunaendelea na matengenezo ya bomba la maji Masingini linalotoa maji kutoka Matangi ya maji Masingini na kupeleka maeneo ya Kianga, Masingini, Mwembe Mchomeke, Mwera, Hawaii na Mtofaani.

Matengenezo hayo yanatarajiwa kukamilika leo jioni ili kurudisha huduma kwa wananchi.

Tunaomba radhi wananchi kwa usumbufu unaoendelea kujitokeza kutokana na kukosa huduma ya maji safi na salama kwa maeneo hayo.

Kitengo cha Uhusiano – ZAWA
Masingini
28 OKTOBA 2026

Address

Mwembe Madema
Zanzibar City

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00

Telephone

+255774778888

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mamlaka ya Maji Zanzibar - ZAWA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Mamlaka ya Maji Zanzibar - ZAWA:

Share

Nearby government services