Ofisi ya Rais - Tamisemim Zanzibar

Directions Website

Ofisi ya Rais - Tamisemim Zanzibar Ukurasa Rasmi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa amesh...
04/10/2026

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa ameshiriki Mkutano wa 8 wa Kamati ya Uratibu ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika El Alamein, Misri.

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo, umeongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius John Ndejembi.

πŸ“† 4 Oct, 2026
πŸ“ El Alamein, Misri

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Issa Mahfoudh Haji amewataka watendaj...
30/09/2026

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Issa Mahfoudh Haji
amewataka watendaji kutumia teknolojia ya TEHAMA katika kurahisisha kazi, kuongeza ufanisi na kuhakikisha taarifa muhimu zinapatikana kwa wakati.

Ameyasema hayo wakati akifungua kikao kazi cha kwanza cha kamati ya uendeshaji wa TEHAMA kilichofanyika katika ukumbi wa mkutano TAMISEMIM Vuga Mkoa wa Mjini Magharibi.

Kikao hicho kimejikita katika kujadili na kuimarisha matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika utoaji wa huduma na utekelezaji wa majukumu ya Serikali.

Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni mfumo wa utambulishaji wa watumishi mfumo wa RSIS (Registrar Societies Information Systems), pamoja na masuala ya kuwasilisha taarifa kwa njia ya kielektroniki na kuboresha mifumo ya taarifa.

Aidha kikao hicho kinatarajiwa kutoa fursa kwa washiriki kujadili changamoto zinazojitokeza katika matumizi ya mifumo hiyo na kuweka mikakati ya kuzitatua ili kuboresha huduma zinazotolewa na Serikali.

πŸ“† 30 Sep, 2026
πŸ“ Vuga, Zanzibar.

25/09/2026
Mwenyekiti wa Tume ya Idara Maalum za SMZ  Mohd Suleiman Ali amewataka Maafisa Utumishi  kuyatekeleza kwa vitendo mafunz...
15/09/2026

Mwenyekiti wa Tume ya Idara Maalum za SMZ Mohd Suleiman Ali amewataka Maafisa Utumishi kuyatekeleza kwa vitendo mafunzo waliopatiwa na kuhakikisha watumishi wote wanapata stahiki zao kwa usawa.

Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya uratibu wa fidia ndani ya idara maalum yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Vuga Wilaya ya mjini.

Amesema hakuna Sababu ya kuwepo kwa tofauti katika utoaji wa fidia kwa watumishi wenye mazingira yanayofanana na kusisisitiza kuwa fidia inapaswa kutumika kwa haki katika vikosi vyote vya Idara Maalum.

Akiendesha mafunzo hayo katibu wa Tume ya Utumishi Idara Maalum za SMZ msaidizi Seif Maabad Makungu amesema Bodi ya Uchunguzi imepewa jukumu la kuchunguza ajali kwa mujibu wa Kanuni za Tume ya Utumishi ya mwaka 2008, ikiwemo kubaini chanzo cha ajali na kiwango cha fidia

Nao maafisa Utumishi Idara Maalum ,wanasheria na madaktari waliopatiwa mafunzo wamesema wameyapokea vyema mafunzo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi kwa mujibu sheria zilizowekwa.

πŸ“† 15 Sept, 2026
πŸ“ Vuga, Zanzibar.

Waziri wa fedha na Mipango Zanzibar  Mhe. Juma Malik Akili amesema mradi wa Big-z unalenga kusaidia kuboresha miundombin...
08/09/2026

Waziri wa fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Juma Malik Akili amesema mradi wa Big-z unalenga kusaidia kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo barabara na Masoko pamoja na kuimarisha huduma za usafi hatua inayolenga kuleta haiba nzuri ya Miji.

Ameyasema hayo katika hafla ya makabidhiano ya Magari ya usafi kati ya Wizara ya fedha na Mipango na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa Magari hayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Idrissa kitwana Mustafa ameishukuru Wizara ya Fedha na Mipango na kuahidi kuwa magari hayo yatakabidhiwa katika maeneo husika na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Aidha Mhe. Idrissa amesema matumizi sahihi ya magari hayo yatasaidia kuimarisha huduma za usafi katika Manispaa za Zanzibar na hivyo kuchangia katika juhudi za Serikali na kuhakikisha Mazingira ya Zanzibar yanakuwa safi na Salama.

Kwa upande wake kaimu katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar ndugu. Aboud Hassan Mwinyi amesema mradi huo unahusisha ununuzi wa magari ya ukusanyaji taka ujenzi wa vizimba pamoja na ujenzi wa vituo vya kuhamishia taka.

Pia mchakato wa ununuzi wa magari umekamilika huku Wizara ikiwa tayari imesaini mkataba kwa ajili ya ujenzi wa vizimba na hatua nyingine za utekelezaji wa mradi zikiendelea.

Jumla ya magari 26 yamekabidhiwa kwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ ambapo magari 15 ni Tipa na magari 11 ni Compactors magari hayo yanatarajiwa kutumika katika Manispaa za Zanzibar kwa ajili ya ukusanyaji na usafirishaji wa taka ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa juhudi za Serikali katika kuboresha usafi wa Mazingira na Afya ya jamii.

πŸ“† 08 Sept, 2026
πŸ“ Vuga, Zanzibar.

Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wajumbe wa Bodi wakipatiwa mafunzo kuhusu taratibu za ununuzi wa umma kat...
05/09/2026

Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wajumbe wa Bodi wakipatiwa mafunzo kuhusu taratibu za ununuzi wa umma katika utekelezaji wa Programu ya Uhimilivu wa Athari za Mabadiliko ya Tabianchi, SCALE Program.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa The Brean of Sau Inn Beach Hotel, Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja, yakilenga kuwajengea uwezo wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ili kufanya maamuzi yanayohusiana na michakato ya ununuzi wa umma katika utekelezaji wa programu hiyo.

Katika mafunzo hayo, washiriki wamepatiwa uelewa kuhusu umuhimu wa kuzingatia Sheria ya Ununuzi wa Umma, kanuni na taratibu zake, pamoja na miongozo ya Benki ya Dunia katika utekelezaji wa shughuli za ununuzi.

Pia mafunzo hayo yanatarajiwa kuongeza ujuzi na uwezo wa Wajumbe wa Bodi na Wakurugenzi katika kusimamia shughuli za ununuzi kwa ufanisi, uwazi na kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.

Aidha, ujuzi huo utasaidia katika utekelezaji bora wa Programu ya SCALE pamoja na miradi mingine inayotekelezwa na Serikali.

πŸ“† 05 Sept, 2026
πŸ“ Jambiani, Zanzibar.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Ndugu Issa Mahfoudh Haji, amewataka...
01/09/2026

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Ndugu Issa Mahfoudh Haji, amewataka wahandisi kuandaa michoro na makisio halisi ya bajeti ya miradi mbalimbali iliyoibuliwa, ili kuhakikisha inatekelezwa kwa ufanisi, uwazi na uwajibikaji.

Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya wahandishi kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa za Unguja na Pemba, yaliyofanyika katika Hoteli ya Visitor’s Inn, Jambiani, Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema miradi hiyo inalenga kupunguza uharibifu wa miundombinu unaosababishwa na mvua kubwa, ukame na athari nyingine za mabadiliko ya tabianchi.

Akiwasilisha mada katika mafunzo hayo, Mhandisi wa Miradi kutoka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini, TARURA, Eng. Thobias Malando, amesema ni muhimu kushirikisha jamii katika hatua za awali za uandaaji wa taarifa na michoro ya miradi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Serikali za Mitaa, Zainab Khamis Kibwana, amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea wahandisi uwezo wa kuibua na kuandaa miradi yenye tija inayozingatia mahitaji ya ya jamii katika kukabilinana Athari za mabadilko ya Tabia nchi,

Nao Wahandisi walioshiriki mafunzo hayo wamesema wamepata ujuzi utakaowasaidia kuandaa michoro na makisio ya gharama kwa usahihi, hatua itakayorahisisha utekelezaji wa mirad hiyo.

Jumla ya miradi 38 iliobuliwa katika Mikoa mbali mbali inatarajiwa kutekelezwa kupitia Program ya Uhimilivu wa Athari za mabadiliko ya Tabianchi (Scale Program) inayofadhiliwa na Benki ya Dunia.

πŸ“† 01 Septemba, 2026
πŸ“ Jambiani, Zanzibar.

Address

Vuga Zanzibar
Zanzibar

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ofisi ya Rais - Tamisemim Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share