15/10/2026
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini Joseph Kilangi ametembelea mradi wa uzalishaji umeme wa kutumia nishati jadidifu ya jua, ulioko Bambi mkoa wa Kusini Unguja
Mradi huo unaotarajiwa kuanza kutumia megawati 7.8 za umeme kuanzia Oktoba 31 kwa ajili ya majaribio ili kupunguza tatizo la uhaba wa umeme nchini.
Amesema kuwa kuna uhaba wa umeme megawati 10 wakati mchana na Usiku katika baadhi ya maeneo hivyo kutumika kwa megawati hizo kutasaidia kupunguza tatizo la umeme.
Katibu amefahamisha kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiliana Saini na Kampuni ya Generation Captal kwa ajili ya kujenga Mradi wa kuzalisha umeme wa jua megawati 180 katika maeneo ya Bambi ambapo megawati hizo zitajengwa kwa awamu ili kupunguza uhaba wa umeme.
Aidha amesema kuwa ameridhishwa na hatua kubwa iliyofikiwa katika kuzalisha umeme huo kwani ni ya mwanzo katika Afrika na ya mwanzo kwa Tanzania kutumia umeme huo.
Katika hatua nyengine Katibu ameishukuru Serikali na Kampuni ya Generation Capital kwa jitihada zake katika kuhakikisha tatizo la umeme linaondoka kabisa nchini.
Hata hivyo amewashukuru wananchi kwa ushirikiano wao na kuwataka kuendelea kuwa wavumilivu.
Meneja wa Mradi huo Steve Wasira ameeleza kuwa Kampuni yao imetiliana Saini ya kujenga megawati 180 ambapo hadi kufikia sasa wameshafikia zaidi ya asilimia 70 ya Miradi huo.
Aidha amesema kuwa katika awamu nyengine wanatarajiwa kuzalisha megawati 20 ifikapo Disemba mwezi huu.