ZBC Zanzibar

Call Directions Website Contact the organization

ZBC Zanzibar Ukurasa Rasmi Wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Mhe. Dkt. Nasra Nassor Omar, amewataka viongozi na watendaji wa Wizara hiyo kufanya k...
06/10/2026

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Mhe. Dkt. Nasra Nassor Omar, amewataka viongozi na watendaji wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano na nia moja ili kutimiza malengo ya Serikali ya kuhakikisha sekta ya Utalii inanufaisha wananchi wote.

Dkt. Nasra ameyasema hayo wakati wa hafla ya makabidhiano ya majukumu ya Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale, iliyofanyika katika ofisi za Wizara hiyo Kikwajuni, Zanzibar.

Amesema mafanikio ya sekta ya Utalii yanapaswa kupimwa kwa kuangalia namna wananchi, ambao ni miongoni mwa wadau wakuu wa sekta hiyo, wanavyonufaika na fursa zinazotokana na utalii.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Mheshimiwa Juma Hassan Thabit, amesema ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ni nguzo muhimu katika kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale, Dkt. Aboud Suleiman Jumbe, amesema sekta ya Utalii ina mchango mkubwa katika Pato la Taifa, hivyo watendaji wanapaswa kuongeza ubunifu na kutumia teknolojia za kisasa ili kuongeza kasi ya ukuaji na ushindani wa sekta hiyo kimataifa.

Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika kufuatia uteuzi wa Dkt. Nasra Nassor Omar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kushika nafasi ya Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale.

Katika hafla hiyo, aliyekuwa Kaimu Waziri wa Wizara hiyo, Mheshimiwa Mudrick Ramadhan Soraga, amekabidhi rasmi majukumu ya Wizara kwa Waziri mpya, Dkt. Nasra Nassor Omar.

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, leo Oktoba 6, 2026 amezindua Mkataba wa Huduma kwa Wateja uliohuishwa p...
06/10/2026

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, leo Oktoba 6, 2026 amezindua Mkataba wa Huduma kwa Wateja uliohuishwa pamoja na huduma mbalimbali za TANESCO zinazolenga kuboresha zaidi namna ya utoaji wa huduma kwa wateja kwa ufanisi na kwa wakati, uzinduzi uliofanyika katika Ukumbi wa Super Dome, jijini Dar es Salaam.

Mhe. Homera amesema matumizi ya mifumo ya teknolojia za kisasa katika utoaji wa huduma kwa wateja yanazidi kuiwezesha TANESCO kupiga hatua kubwa katika kuboresha huduma zake kwa kuzingatia uwajibikaji, uwazi na weledi unaolenga kuleta matokeo chanya kiutendaji.

Ametoa rai kuhakikisha changamoto zinazowakabili wananchi katika matumizi ya umeme zinashughulikiwa kwa haraka kwa kuwa changamoto katika huduma ya umeme zinaweza kuathiri moja kwa moja uzalishaji na shughuli za kiuchumi.

“Mwelekeo wa Serikali ni kujenga sekta ya nishati inayoweza kuunga mkono kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania. Tunataka kuona shughuli za uzalishaji zinaendelea bila vikwazo visivyo vya lazima na tunataka wananchi wapate huduma kwa urahisi zaidi,” ameeleza Waziri Homera.

Amesema Tanzania hivi sasa ina umeme wa kutosha, ambapo uwezo wa uzalishaji umefikia jumla ya Megawati 4,606 dhidi ya mahitaji ya juu ya Megawati 2,316, hatua inayotoa fursa zaidi za kukuza shughuli za kiuchumi kupitia uwekezaji katika viwanda, biashara na shughuli za kijamii.

Kikosi cha Zanzibar Spice Boys chenye wachezaji chipukizi 18, leo alfajiri kimewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataif...
06/10/2026

Kikosi cha Zanzibar Spice Boys chenye wachezaji chipukizi 18, leo alfajiri kimewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Belo Horizonte/Confins–Tancredo Neves International, nchini Brazil, tayari kwa kushiriki mashindano ya kimataifa ya soka la watoto ya PQCUPBRASIL 2026.

Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 10 hadi 15 Oktoba 2026 katika jimbo la Minas Gerais, Brazil. Kikosi hicho kinaongozwa na Mkuu wa Msafara, Mhe. Balozi Abdulsamad Abdulrahim, ambaye ni Balozi wa Heshima wa Brazil mstaafu.

Zanzibar Spice Boys watashiriki katika Kundi A la U-13, pamoja na timu za Clube Minas Gerais, Soccer Pro Betim, Polo Novo Horizonte Rio Vermelho, Vitinho Soccer Itabira na FC Porto ya Ureno.

Ushiriki wa Zanzibar Spice Boys katika mashindano hayo unatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kuitangaza Zanzibar kupitia vipaji vya watoto, utamaduni, utalii na maendeleo ya michezo, huku ukitoa fursa kwa vijana hao kupata uzoefu wa kushindana katika jukwaa la kimataifa.

06/10/2026

Ujenzi wa Uwanja wa Fumba, ambao ni miongoni mwa miradi mikubwa ya miundombinu ya michezo inayotekelezwa kupitia mradi wa Zanzibar Sports City, umefikia asilimia 86 ya utekelezaji.

Uwanja huo unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 31, 2026, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Zanzibar kuwa na miundombinu ya kisasa ya michezo, huku ukitarajiwa kutumika katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, zinazotarajiwa kufanyika Juni 2027 katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

Uwanja wa Fumba umejengwa kwa kuzingatia viwango vya kisasa, ukiwa na miundombinu mbalimbali ikiwemo vyumba vya mikutano, gym, vyoo vya kisasa, maduka ya biashara, pamoja na vyumba maalum vya wachezaji na waamuzi kwa ajili ya kubadilisha nguo.

Mradi huo unatarajiwa kuongeza uwezo wa Zanzibar kuwa mwenyeji wa matukio makubwa ya michezo na kutoa mazingira bora kwa wanamichezo, mashabiki na wadau mbalimbali.

Sikiliza kipindi cha CHAPUO kupitia ZBC Radio, tukikuletea uchambuzi wa Mada,Mikasa Uswahilini, Happy birthday, Habari k...
06/10/2026

Sikiliza kipindi cha CHAPUO kupitia ZBC Radio, tukikuletea uchambuzi wa Mada,Mikasa Uswahilini, Happy birthday, Habari kwa Ufupi na Mapishi

🎙Dj Faza, Khadija Hassan Vuai na Asha Hamad

Tunapatika kupitia Unguja 90.6 MHz Pemba 94.1 MHz kuanzia saa 4 kamili hadi saa 6 kamili

Umetazama leo kipindi cha Asubuhi Njema? K**a hujatazama, kipindi kizima kipo kwenye YouTube Channel ya ZBC Zanzibar.🎙Am...
06/10/2026

Umetazama leo kipindi cha Asubuhi Njema? K**a hujatazama, kipindi kizima kipo kwenye YouTube Channel ya ZBC Zanzibar.

🎙Amina Mkombe, More Six Moh'd, Godfrey Hussein na


Kurasa za juu za Magazeti ya leo Oktoba 06 2026.
06/10/2026

Kurasa za juu za Magazeti ya leo Oktoba 06 2026.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, amesema Tanzania na Misri zitaendelea kuimarisha us...
05/10/2026

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, amesema Tanzania na Misri zitaendelea kuimarisha ushirikiano katika kukabiliana na usafirishaji haramu wa binadamu pamoja na magendo ya wahamiaji.

Mhe. Ayoub amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa maofisa kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali, yanayolenga kuwajengea uwezo katika mapambano dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu.

Amesema ushirikiano wa kimataifa ni muhimu katika kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka, hususan katika kubadilishana taarifa, uzoefu na mbinu za kiutendaji. Ameongeza kuwa jumla ya maofisa, wakaguzi na askari 69 kutoka Tanzania wamepata mafunzo nchini Misri katika kipindi cha mwaka 2024 hadi 2025.

Naibu Waziri amesisitiza kuwa changamoto za uhamaji wa watu na kuongezeka kwa mitandao ya uhalifu inayojihusisha na usafirishaji haramu wa binadamu zinahitaji nchi kuendelea kushirikiana kwa karibu, huku akiwataka washiriki kutumia maarifa watakayoyapata katika mafunzo hayo kulinda wahanga na kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Riziki Pembe Juma, ameshiriki katika hafla ya uapisho wa ...
05/10/2026

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Riziki Pembe Juma, ameshiriki katika hafla ya uapisho wa Mawaziri na Naibu Mawaziri, iliyofanyika leo tarehe 05 Oktoba 2026 katika Ikulu ya Zanzibar.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Amani Abeid Karume, amehudhur...
05/10/2026

Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Amani Abeid Karume, amehudhuria hafla ya uapisho wa Mawaziri na Naibu Mawaziri, iliyofanyika leo tarehe 05 Oktoba 2026 katika Ikulu ya Zanzibar.

Address

Zanzibar
Zanzibar
70001

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ZBC Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to ZBC Zanzibar:

Shortcuts

Share