Mahkama ya Zanzibar

Directions Website

Mahkama ya Zanzibar Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Mahkama ya Zanzibar, Government Organization, BOX NO 160, ZANZIBAR, Zanzibar.

Mke wa Jaji Mkuu wa Malawi, Bi. Mary Carolyn Mzikamanda, pamoja na Mke wa Jaji Mkuu wa Zambia, Bi. Mwiza Helen Nzila Mal...
09/10/2026

Mke wa Jaji Mkuu wa Malawi, Bi. Mary Carolyn Mzikamanda, pamoja na Mke wa Jaji Mkuu wa Zambia, Bi. Mwiza Helen Nzila Malila, wamepata fursa ya kutembelea kituo cha Zanzibar Children Rehabilitation Organization kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wenye mahitaji maalumu wanaolelewa katika kituo hicho.

Katika ziara hiyo, wageni hao walitoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa lengo la kuwafariji watoto na kuchangia katika kukidhi mahitaji yao. Ziara hiyo pia ilikuwa fursa ya kuonesha upendo, kujenga ukaribu na watoto hao na kuthamini juhudi zinazofanywa katika kuwalea na kuwahudumia.

Aidha, walitembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria na vivutio vya utalii vilivyopo Zanzibar, yakiwemo Hifadhi ya Msitu wa Jozani, Mji Mkongwe na Kanisa la Mkunazini. Ziara katika maeneo hayo iliwapa nafasi ya kufahamu zaidi historia, utamaduni na urithi wa Zanzibar, pamoja na kujionea uzuri wa mazingira na vivutio vyake vya kipekee..

Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan, amejumuika na wageni wake katika hafla ya chakula cha usiku kwa Majaji Waku...
08/10/2026

Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan, amejumuika na wageni wake katika hafla ya chakula cha usiku kwa Majaji Wakuu wa nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika pamoja na viongozi wengine wa Mahakama.

WAJUMBE WA MKUTANO WA MAJAJI WAKUU WATEMBELEA VIVUTIO VYA ZANZIBARWajumbe wa Mkutano wa Majaji Wakuu wa Nchi za Kusini n...
07/10/2026

WAJUMBE WA MKUTANO WA MAJAJI WAKUU WATEMBELEA VIVUTIO VYA ZANZIBAR

Wajumbe wa Mkutano wa Majaji Wakuu wa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEACJF), leo tarehe 7 Oktoba 2026, wamepata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria na vivutio vya utalii vilivyopo Zanzibar.

Ziara hiyo imewapa wajumbe fursa ya kujionea urithi wa kihistoria na kiutamaduni wa Zanzibar, pamoja na kufahamu zaidi kuhusu vivutio vinavyoifanya Zanzibar kuwa miongoni mwa maeneo maarufu ya utalii katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Mbali na kushiriki mijadala kuhusu masuala ya utoaji haki, ziara hiyo imekuwa sehemu ya programu ya mkutano inayolenga kuwapa wajumbe nafasi ya kuifahamu Zanzibar, historia yake, utamaduni wake na vivutio vyake mbalimbali.

Mkutano wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEACJF) unafanyika Zanzibar kuanzia tarehe 5 hadi 8 Oktoba 2026.

07/10/2026

JAJI MKUU WA ZANZIBAR AWATAKA MAJAJI WAKUU WA AFRIKA KUTUMIA MIKUTANO YA KIKANDA KUCHOCHEA MABORESHO YA MIFUMO YA UTOAJI HAKI

Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla, amewataka Majaji Wakuu na viongozi wa Mahkama za kusini Mashariki mwa Afrika kuhakikisha kuwa mafunzo, uzoefu na maazimio yanayopatikana katika mikutano ya kikanda yanatafsiriwa kuwa hatua za vitendo zitakazochochea maboresho ya mifumo ya utoaji haki.

Mhe. Jaji Mkuu ameyasema hayo tarehe 6 Oktoba 2026, wakati akifunga h Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEACJF), uliofanyika katika Hoteli ya Verde, Zanzibar.

Amesema mkutano huo umetoa fursa muhimu kwa Majaji Wakuu, Majaji, Mahakimu na viongozi wengine wa Mahakama kutoka nchi mbalimbali kubadilishana uzoefu, kujifunza mbinu bora na kuendeleza fikra za kisheria katika usimamizi na utoaji wa haki.

Amesisitiza kuwa thamani halisi ya mijadala hiyo itaonekana pale ambapo maarifa, uzoefu na mawazo yaliyoshirikishwa yataweza kutafsiriwa kuwa maboresho yanayoonekana katika Mahakama za nchi wanachama. Ameongeza kuwa Mahakama zinapaswa kuendelea kujenga uwezo wa watendaji wake na kuandaa mipango ya utekelezaji inayozingatia mahitaji yanayobadilika ya Mahakama na jamii wanazozihudumia.

Amesema hatua hizo zitasaidia kujenga Mahakama zinazowajibika zaidi, zenye ufanisi, zinazofikika kwa urahisi kwa wananchi na zenye uwezo wa kutoa haki kwa wakati na kwa ubora, huku zikilinda imani ya wananchi na kuimarisha utawala wa sheria.

Aidha, amewataka viongozi wa Mahakama kuhakikisha kuwa maazimio yaliyofikiwa katika mkutano huo yanatekelezwa katika taasisi zao, akisisitiza kuwa nguvu ya Mahakama haipo katika maamuzi yake pekee, bali pia katika uadilifu, uhuru, usawa, ufanisi na upatikanaji sawa wa haki kwa wote.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEACJF) ambaye pia ni Jaji Mkuu wa Kenya, Mhe. Martha Koome, amesema mkutano huo umewakumbusha washiriki kuwa Mahkama si sehemu za kusikiliza na kuamua mashauri pekee, bali ni taasisi zinazotegemea ushirikiano wa wataalamu wa kada mbalimbali ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Aidha, amesema uhuru wa Mahakama haupaswi kuishia katika uhuru wa kufanya maamuzi ndani ya vyumba vya Mahkama pekee, bali unapaswa pia kuambatana na uwezo wa taasisi hizo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Amesisitiza kuwa Mahkama zinapaswa kuwa na rasilimali za kutosha zinazopatikana kwa wakati, pamoja na kuwa na uwezo wa kupanga vipaumbele na kusimamia rasilimali hizo kwa uwazi na uwajibikaji.

Mkutano huo uliwakutanisha Majaji Wakuu, Majaji, viongozi na watendaji wa Mahakama kutoka nchi mbalimbali za Kusini na Mashariki mwa Afrika kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kujadili mikakati ya kuimarisha mifumo ya utoaji haki katika ukanda huo.

Masuala mbalimbali ya yalijadiliwa katika mkutano huo, yakiwemo uhuru wa kifedha wa Mahakama, Usuluhishi Mbadala wa Migogoro (ADR), matumizi ya Akili Bandia (AI), mageuzi ya kidijitali katika Mahakama, usimamizi wa Mahakama pamoja na uboreshaji wa mifumo ya utoaji haki.

Wajumbe wa  Mkutano wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEACJF) wakiendelea na mkutano ...
06/10/2026

Wajumbe wa Mkutano wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEACJF) wakiendelea na mkutano wao unaofanyika katika Hoteli ya Verde, Zanzibar, kuanzia tarehe 5 hadi 9 Oktoba 2026.

Mkutano huo unawakutanisha viongozi wa Mahkama kutoka nchi mbalimbali kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kujadili masuala muhimu yanayohusu sekta ya haki, pamoja na kuimarisha ushirikiano katika kuboresha mifumo ya utoaji haki

05/10/2026
RAIS MWINYI  UJIO WA MAJAJI WAKUU WA MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA ZANZIBAR NI ISHARA YA AMANI, UONGOZI BORA NA MSHIKAM...
05/10/2026

RAIS MWINYI UJIO WA MAJAJI WAKUU WA MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA ZANZIBAR NI ISHARA YA AMANI, UONGOZI BORA NA MSHIKAMANO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kufanyika kwa Mkutano wa Majaji Wakuu wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (SEACJF) Zanzibar ni ishara ya uwepo wa amani, uongozi bora na mshikamano, pamoja na kuimarika kwa ushirikiano baina ya nchi za Afrika.

Rais Mwinyi ameyasema hayo wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEACJF), unaofanyika katika Hoteli ya Verde, Mtoni, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja, kuanzia tarehe 5 hadi 9 Oktoba 2026.

Amesema uwepo wa Majaji Wakuu na viongozi waandamizi wa Mahkama kutoka nchi mbalimbali za ukanda huo unatoa fursa muhimu ya kuimarisha umoja na ushirikiano, pamoja na kubadilishana uzoefu na kujifunza mbinu bora za kuboresha mifumo ya utoaji haki.

Rais Mwinyi ameeleza kuwa mkutano huo ni jukwaa muhimu kwa nchi wanachama kujadili mageuzi ya kimahakama, kuimarisha ufanisi katika utoaji wa haki na kutafuta suluhisho la pamoja dhidi ya changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya haki barani Afrika.

Aidha, amesema majadiliano ya mkutano huo yanatarajiwa kutoa mchango mkubwa katika kukabiliana na changamoto mbalimbali, ikiwemo uhalifu wa kiuchumi, ambao umeendelea kuwa miongoni mwa changamoto zinazozikabili nchi nyingi, hususan barani Afrika.

Amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano baina ya nchi, hususan katika mifumo ya sheria na Mahkama, ili kuwezesha mapambano dhidi ya uhalifu wa kiuchumi na aina nyingine za uhalifu unaovuka mipaka kufanyika kwa ufanisi zaidi.

Vilevile, Rais Mwinyi amesisitiza umuhimu wa uhuru wa Mahkama, akieleza kuwa Mahakama huru ni nguzo muhimu katika kuhakikisha haki inatolewa kwa mujibu wa sheria, bila upendeleo wala kuingiliwa, na hivyo kuimarisha imani ya wananchi katika mfumo wa utoaji haki.

Rais Mwinyi amehakikishia washiriki kuwa Zanzibar itaendelea kuunga mkono juhudi na mipango inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kikanda, utawala wa sheria na maendeleo ya mifumo ya haki, kwa manufaa ya wananchi wa Afrika na dunia kwa ujumla.

Naye Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla, amesema ushirikiano baina ya Majaji Wakuu wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika una umuhimu mkubwa katika kuimarisha uwajibikaji ndani ya taasisi za Mahakama, kuongeza ufanisi wa mifumo ya utoaji haki na kuharakisha upatikanaji wa haki kwa wananchi.

Mhe. Jaji Mkuu amesema mkutano huo unatoa fursa muhimu kwa Mahakama za nchi wanachama kujadili mageuzi yanayoendelea katika sekta ya haki, yakiwemo matumizi ya teknolojia katika uendeshaji wa Mahakama, usimamizi wa mashauri na uboreshaji wa huduma zinazotolewa kwa wananchi.
Aidha, amesema Zanzibar itanufaika na uzoefu wa nchi mbalimbali kupitia majadiliano na kubadilishana maarifa, pamoja na kujifunza mbinu bora zinazotumika katika uendeshaji na usimamizi wa Mahakama.

Ameeleza kuwa mikutano ya aina hiyo ni muhimu kwa kuwa inawakutanisha viongozi wa Mahakama kujadili changamoto zinazofanana katika mifumo ya utoaji haki na kutafuta kwa pamoja suluhisho na mikakati madhubuti ya kukabiliana nazo.
Mhe. Jaji Mkuu amesisitiza kuwa ushirikiano huo utaendelea kuwa nyenzo muhimu katika kuimarisha utawala wa sheria, kuongeza ufanisi na uwajibikaji wa Mahakama, pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa wakati na kwa usawa.

WATENDAJI WAKUU WA MAHAKAMA ZA KUSINI NA MASHARIKI MWA AFRIKA WAKUTANA ZANZIBARWatendaji Wakuu wa Mahakama kutoka nchi z...
04/10/2026

WATENDAJI WAKUU WA MAHAKAMA ZA KUSINI NA MASHARIKI MWA AFRIKA WAKUTANA ZANZIBAR

Watendaji Wakuu wa Mahakama kutoka nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika, kupitia Southern and Eastern Africa Judicial Administrators Association (SEAJAA), leo tarehe 4 Oktoba 2026, wamekutana Zanzibar kwa kikao kazi kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya utawala na uendeshaji wa Mahakama, pamoja na kubadilishana uzoefu kuhusu namna bora ya kuboresha utoaji wa huduma za haki kwa wananchi.

Kikao hicho, kilichofanyika katika Hoteli ya Verde, Zanzibar, kimetoa fursa kwa washiriki kujadili mikakati ya kuimarisha utendaji wa Mahakama, kuongeza ufanisi, kukuza matumizi ya teknolojia na ubunifu, pamoja na kuboresha mifumo ya utawala wa Mahakama kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma za haki kwa wananchi.

SEAJAA inawakutanisha watendaji wa Mahakama kutoka nchi mbalimbali za Kusini na Mashariki mwa Afrika, zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Botswana, Eswatini, Lesotho, Malawi, Mauritius, Mozambique, Namibia, Seychelles, Afrika Kusini, Zambia na Zimbabwe na Zanzibar kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, kubadilishana uzoefu na kukuza ufanisi katika usimamizi na uendeshaji wa Mahakama.

Aidha, Watendaji Wakuu hao wanatarajiwa kushiriki katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEACJF), utakaofanyika Zanzibar kuanzia tarehe 5 hadi 9 Oktoba 2026.

Mkutano huo wa SEACJF unatarajiwa kuwakutanisha Majaji Wakuu na viongozi waandamizi wa Mahakama kutoka nchi wanachama kwa ajili ya kujadili masuala ya pamoja yanayohusu maendeleo ya sekta ya haki, mageuzi ya Mahakama na kuimarisha ushirikiano wa kimahakama katika ukanda wa Kusini na Mashariki mwa Afrika.

Address

BOX NO 160, ZANZIBAR
Zanzibar
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mahkama ya Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share