fetatanzania

Website

fetatanzania Fisheries Education and Training Agency (FETA). Ukurasa Rasmi wa Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi. Excellency in Fisheries.

BENKI YA DUNIA YAIPONGEZA FETA KWA UTEKELEZAJI WA MRADI WA TASFAM.Pongezi hizo zimetolewa 26 Oktoba, 2026 na Ujumbe Kuto...
26/10/2026

BENKI YA DUNIA YAIPONGEZA FETA KWA UTEKELEZAJI WA MRADI WA TASFAM.

Pongezi hizo zimetolewa 26 Oktoba, 2026 na Ujumbe Kutoka Benki ya Dunia ukiongozwa na Task Team Leader Bw. Mirko Ivo Serkovic kwenye kikao cha pamoja kilichohusisha ujumbe toka Benki ya Dunia, Timu ya wataalamu wa Mradi wa Kukuza Usimamizi Endelevu wa Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji Bahari Tanzania (TASFAM) kutoka wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na FETA kwa lengo la kujadili utekelezaji wa mradi wa TASFAM, FETA.

Kwenye kikao hiko, Mtendaji Mkuu wa FETA Dkt Semvua Mzighani aliielezea Taasisi ya FETA na majukumu yake kwa ufupi kisha Mratibu wa Mradi wa TASFAM, FETA Bw. Arnold Mbunda alielezea utekelezaji wa mradi wa TASFAM kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Kupitia mradi wa TASFAM, FETA imewezesha mafunzo ya muda mfupi kwa mabaharia na waendeshaji wa vyombo baharini juu ya usalama majini,Mafunzo ya uchakataji mazao ya uvuvi na mwani yamefanyika. Imewezesha zoezi la uhuishaji wa mitaala 5 na uanzishwaji wa mitaala mipya 12, Imewezesha mafunzo ya matengenezo na utunzaji wa boti na injini za uvuvi kwa washiriki 40 kutoka Mikoa ya Tanga na Lindi.
Miongozo 8 ya mafunzo ya muda mfupi imeandaliwa, Mitaala kwaajili ya mabaharia STCW imeandaliwa, Watumishi wamejengewa uwezo kupata mafunzo mbalimbali hasa matumizi ya vifaa vya maabara

Kikao hiko pia kilihudhuriwa na Mratibu wa Mradi wa Uendelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji Tanzania (TASFAM) kwa upande wa Tanzania bara Dkt. Nichrous Mlalila

Baada ya kikao Ujumbe wa Benki ya Dunia ulipata fursa ya kutembelea idara ya Ukuzaji viumbe maji na kujionea uzalishaji wa vifaranga vya samaki aina ya sato na mabwawa ya kufugia samaki.

Nyote mnakaribishwa.
16/10/2026

Nyote mnakaribishwa.

Bodi ya ushauri ya Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA ) chini ya Mwenyekiti wake Dkt. Blandina Lugendo  imeketi 1...
16/10/2026

Bodi ya ushauri ya Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA ) chini ya Mwenyekiti wake Dkt. Blandina Lugendo imeketi 15 Oktoba,2026 kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Wakala.

Pamoja na mambo mengine Bodi imepitia na kushauri taarifa ya Mtendaji Mkuu wa FETA iliyokuwa na sehemu tatu Taarifa ya mendeleo ya taaluma, Taarifa ya masuala ya kiutawala pamoja na Taarifa ya fedha.

Baada ya kikao hiko Wajumbe wa bodi walipata fursa ya kutembelea sehemu ya uzalishaji wa vifaranga vya samaki, ukuzaji wa samaki wazazi na mabwawa ya kufugia samaki aina ya sato na kambale.

FETA YAHITIMISHA MAFUNZO YA UONGOZI WA JAMII KATIKA UHIFADHI WA RASILIMALI ZA PWANI NA BAHARI. Wakala ya Elimu na Mafunz...
28/09/2026

FETA YAHITIMISHA MAFUNZO YA UONGOZI WA JAMII KATIKA UHIFADHI WA RASILIMALI ZA PWANI NA BAHARI.


Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Tarehe 27 Septemba, 2026 imehitimisha mafunzo ya muda mfupi ya Uongozi wa Jamii katika Uhifadhi wa Rasilimali za Pwani na Bahari (Conservation Leadership Training Programme) yaliyolenga kuwawezesha viongozi na wadau wa jamii kushiriki kikamilifu katika usimamizi na uhifadhi endelevu wa rasilimali za pwani na bahari.

Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Kampasi ya FETA Mbegani, Bagamoyo, kwa siku 14 kuanzia 14–27 Septemba, 2026 yakishirikisha washiriki 20 kutoka Tanga na Pemba yamefadhiliwa na Ubalozi wa Ireland Tanzania kupitia IUCN Tanzania, huku FETA ikiwa mshirika wa utekelezaji katika kujenga uwezo wa washiriki wanaohusika na usimamizi, matumizi na uhifadhi wa rasilimali za pwani na bahari.

Akifunga mafunzo hayo, Kaimu Mtendaji Mkuu wa FETA, Bw. Deus J. Bwathondi, amewataka washiriki kutumia maarifa na ujuzi walioupata kuleta matokeo chanya katika jamii zao. Alisisitiza kuwa mafunzo hayo hayapaswi kuishia kwa washiriki pekee, bali yawe chachu ya kuwafikia wananchi na vikundi vinavyohusika na matumizi na usimamizi wa rasilimali za pwani na bahari.

“Ninyi mliopata mafunzo haya msiwe walengwa pekee wa maarifa haya. Mnapaswa kuwa walimu na wawezeshaji katika jamii zenu, mkawafikishie wengine ujuzi mliojifunza ili kuongeza uelewa na kuimarisha usimamizi na uhifadhi wa rasilimali za pwani na bahari,” alisema Bw. Bwathondi.

Aidha amebainisha kuwa FETA itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kujenga uwezo wa jamii katika uhifadhi, usimamizi endelevu na matumizi yenye tija ya rasilimali za pwani na bahari, sambamba na kuchangia utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya taifa na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa IUCN, Bw. Joseph Olila, aliwataka washiriki kuwa mabalozi wa uongozi bora, usimamizi na matumizi endelevu ya rasilimali za pwani na bahari katika maeneo yao. Pia aliipongeza FETA kwa kutoa mafunzo hayo na kusisitiza umuhimu wa kujenga uwezo wa viongozi na wadau wa jamii katika kuimarisha uhifadhi wa rasilimali za bahari huku akiahidi kuwa IUCN itaendelea kushirikiana na FETA.

PROF. SHEIKH ATAKA MITAALA YA FETA IENDANE NA MAHITAJI YA DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050.Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya...
25/09/2026

PROF. SHEIKH ATAKA MITAALA YA FETA IENDANE NA MAHITAJI YA DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Prof. Mohammed Sheikh ametaka Mitaala inayohuishwa na inayopendekezwa kuanzishwa na Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kuendana na mahitaji ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2050.

Prof. Sheikh ametoa kauli hiyo 25 Septemba, 2026 alipokuwa anafungua kikao cha kuwasilisha Rasimu ya mitaala iliyohuishwa na inayopendekezwa kuanzishwa na FETA kwenye Menejimenti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kilichofanyika Mtumba, Dodoma.

Amebainisha kwamba zoezi hili la uhuishaji na uanzishaji wa mitaala mipya ni muhimu kwa wakati huu sababu kuna mabadiliko makubwa ya sera, sayansi, teknolojia na diplomasia ya masoko ya ndani na ya kimataifa, hivyo mitaala lazima iendane na mabadiliko yaliyopo sasa.

Aidha amesema kuwa mabadiliko haya ya mitaala ni lazima yaendane na mafunzo kwa wakufunzi wa FETA hasa kwa kupitia kubadilishana uzoefu na vyuo vingine, hususan vya nje ya nchi ili waweze kuendana na mabadiliko ya teknolojia yaliyopo hivi sasa.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa FETA Dkt. Semvua Mzighani amesema kwamba mitaala hii itakapoanza kutumika itaongeza fursa zipatikanazo toka katika Uchumi wa Buluu na hivyo kuongeza ajira, uhakika wa chakula, uhifadhi wa mazingira na Pato la Taifa kwa ujumla.

Mitaala inayohuishwa na inayopendekezwa kuanzishwa na FETA inajumuisha matumizi ya teknolojia za kisasa k**a vile Akili Unde (Artificial Intelligence), Mtandao wa Vitu (Internet of Things) na ndege nyuki (Drones).

Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kampasi ya Nyegezi, Mwanza Tar 24 Septemba,2026 yapokea  ugeni kutoka  Shirik...
25/09/2026

Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kampasi ya Nyegezi, Mwanza Tar 24 Septemba,2026 yapokea ugeni kutoka Shirika la Maendeleo la Japan JICA kwaajili ya maandalizi ya mradi wa "Comanagement model for sustainable fisheries resource utilization by integrating cutting edge genomic science and community-based innovation" (SATREP Project).

FETA itakuwa ni miongoni mwa wadau watakaoshiriki katika kutekeleza mradi huo unaotarijiwa kutekelezwa katika mikoa ya kanda ya ziwa Victoria.

24/09/2026
FETA YAZINDUA MAFUNZO YA UZALISHAJI WA VIFARANGA VYA SAMAKI MOROGORO NA MWANZA.Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA...
23/09/2026

FETA YAZINDUA MAFUNZO YA UZALISHAJI WA VIFARANGA VYA SAMAKI MOROGORO NA MWANZA.

Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kwa ufadhili wa Shirika la World Fish tarehe 23 Septemba, 2026 imezindua mafunzo ya siku 4 kuhusu uzalishaji wa vifaranga vya samaki aina ya Sato na Kambale Mkoani Morogoro na Jijini Mwanza.

Mafunzo haya yamehusisha washiriki 54 ambapo 30 wanapatiwa mafunzo katika Kituo cha Ukuzaji Viumbe Maji Kingolwira, Morogoro na washiriki 24 wanapatiwa mafunzo Kampasi ya FETA Nyegezi, Mwanza.

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Ukuzaji Viumbe Maji Wizara ya Mifugo na uvuvi, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Ukuzaji Viumbe Maji Bi Janeth Rukanda amesema mahitaji ya vifaranga bora vya samaki ni makubwa kulingana nahali ya uzalishaji wa sasa na ukuaji wa teknolojia. Hivyo mafunzo haya ni msingi endelevu wa utakaowezesha kuzalisha vifaranga bora na vya kutosha.

"Tunatarajia baada ya mafunzo haya tutaongeza upatikanaji wa vifaranga bora vya samaki pamoja na kusambaza teknolojia ya utotoleshaji ili kuendana na ukuaji wa teknolojia" Amesema Bi Rukanda.

Naye Naibu Mkuu wa FETA Bi Merisia Mparazo kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa FETA amesema kuwa mafunzo haya yana umuhimu mkubwa katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 ambayo inasisitiza kujenga uchumi wenye tija, ushindani, na utengenezaji wa ajira kwa wananchi kupitia sekta zalishaji ikiwemo Sekta ya Uvuvi.

Aidha, amewashukuru Worldfish kwa kuendelea kushirikiana na Feta kutekeleza masuala mbalimbali ikiwemo kuwezesha mafunzo haya yanayokwenda kuleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya ufugaji samaki.

Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo haya Bw Mashaka Kapagalla amesema kuwa mafunzo haya ni mwendelezo wa mafunzo yaliyofanyika Kampasi ya FETA Mbegani mwezi Februari 2026 na kuhusisha washiriki 32 kupitia ufadhili wa Worldfish chini ya Mradi wa Fish Compact. Lengo la mradi ni kuwafikia washiriki 1,500 nchini ambapo hadi sasa washiriki 86 wamefikiwa.

Washiriki wanapatiwa ujuzi wa utunzaji wa samaki wazazi, uzalishaji na utunzaji wa vifaranga vya samaki pamoja na usimamizi wa vitotoleshi vya samaki aina ya Sato na Kambale.

WASHIRIKI WA MAFUNZO YA UFUGAJI SAMAKI MKOANI KIGOMA WAMETAKIWA KWENDA KUZALISHA SAMAKI.Rai hiyo imetolewa 14 Septemba, ...
14/09/2026

WASHIRIKI WA MAFUNZO YA UFUGAJI SAMAKI MKOANI KIGOMA WAMETAKIWA KWENDA KUZALISHA SAMAKI.

Rai hiyo imetolewa 14 Septemba, 2026 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Bw. Hassan Rugwa Wakati akifunga mafunzo ya wiki nne kwa washiriki 57 wa mafunzo ya ufugaji samaki yaliyoendeshwa Mkoani Kigoma na Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Kampasi ya Kigoma kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Ubegiji Enabel kupitia mradi wa wezesha binti.

Bw. Rugwa amesema mafunzo waliopata washiriki hawa yawe chachu kwa wao kwenda kufanya shughui za uzalishaji, ufugaji na uchakataji wa samaki kwani Taifa linawategemea waweze kuongeza tija katika sekta ya ufugaji samaki.

Naye Mtendaji Mkuu wa FETA Dkt. Semvua Mzighani ambao ndio walioendesha mafunzo hayo amesema kuwa mafunzo haya ni kipaumbele cha Taifa kwa hivi sasa kwani serikali inaweka mkazo katika ukuzaji wa viumbe maji na ufugaji wa samaki.

Kwa upande wake Meneja wa FETA kampasi ya Kigoma Bw August Shirima amesema Mafunzo haya yalianza tarehe 17 Agosti mpaka tarehe 11 September 2026 ambapo washiriki kutoka Halmashauri ya kigoma vijijini na Manispaa ya kigoma Ujiji walipata mafunzo ya darasani kwa wiki mbili na mafunzo ya vitendo kwa wiki mbili.

Aidha amebainisha kuwa lengo ni kuwafikia washiriki 200 ambapo mpaka sasa washiriki 151 wameshafikiwa ambapo 84 ni wafugaji samaki na 67 ni wachakataji wa mazao ya samaki.

Naye Mwakilishi wa Enabel ambao ndio wafadhili wa mradi huu Bw. Magesa Mwangwa amesema wamefadhili mafunzo haya lengo kuwajengea uwezo vijana kuweza kujiajiri na kuajiriwa katika vituo mbalimbali vya ufugaji na uchakataji wa samaki.

Kwa upande wao washiriki waliopata mafunzo haya wameiomba serikali kuwawezesha mitaji ili waweze kujiajiri wenyewe katika sekta ya ufugaji samaki.

Mafunzo haya yataongeza uwezo wa vijana kushiriki kikamilifu katika mnyororo wa thamani wa uvuvi na ukuzaji viumbe maji,kuongeza fursa za ajira na kujiajiri pamoja na kuwawezesha kuanzisha na kuendesha shughuli za kiuchumi zinazohusiana na sekta ya uvuvi na ufugaji wa samaki.

Address

FETA, P. O. BOX 83
Bagamoyo

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when fetatanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share