Idara ya Habari Maelezo Zanzibar

Call Directions Website Contact the organization

Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Idara ya Habari Maelezo Zanzibar (DIS), Ipo chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Sehemu ya Utumishi na Uendeshaji
2. Sehemu ya Ufundi
5.

Idara ya Habari Zanzibar (ZIS) ni Idara chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo . Idara ya Habari MAELEZO Zanzibar inajukumu la kutoa taarifa kuhusu Sera, Mipango na utekelezaji wa miradi ya Maendeleo mbalimbali ya Serikali kwa wananchi. Idara imeanzishwa mwaka 1996 baada ya kutenganishwa kwa Sauti ya Tanzania Zanzibar ambayo sasa ni Shirika la Utangazaji Zanzibar kutoka Idara ya Habari na Utangazaji iliyoundwa baada ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964. Kwa sasa Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO ni Hassan Vuai na Naibu Mkurugenzi ni Dk Juma Mohammed Salum. Kimuundo wa Utawala, Idara imegawika sehemu tano(5) ambazo ndizo zinazounda Kamati ya Uongozi ya Idara k**a ifuatavyo:-
1. Sehemu ya Habari (Editorial)
3. Usajili wa Magazeti na Majarida
4. Sehemu ya Hesabu


S
MAJUKUMU YA IDARA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
Majukumu ya Idara hii ni pamoja na :-
1. Kuwa msemaji wa mambo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
2. Kuiwekea Serikali kumbukumbu katika kutayarisha na kutoa vielelezo vya sinema, video, majarida, vitabu vya taaluma, tamthilia na burudani.
3. Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Habari ya Zanzibar na sheria Na. 5 ya mwaka 1988 inayohusiana na mambo ya vitabu na Magazeti
4. Kutetea msimamo wa Serikali katika kupambana na habari na tuhuma zinazotolewa na vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi dhidi ya Serikali
5. Kuishauri Serikali kuhusu nyendo za vyombo vya habari na kupendekeza hatua muafaka za kuchukuliwa
6. Kusimamia, kutoa au kuzuia vibali vya uanzishwaji wa magazeti na majarida mbalimbali Zanzibar
7. Kusimamia kutoa vitambulisho kwa waandishi wa Habari na wapigapicha wa ndani na nje ya Zanzibar watakaofanya kazi Zanzibar
8. Kuwaelekeza waandishi wa habarui watakaofanyakazi hapa Zanzibar maadili, maeneo na mipaka yao na utendaji

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina mpango wa kuzuia uingizaji wa bidhaa chakavu za umeme (used) kutoka nje ya nchi il...
30/10/2026

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina mpango wa kuzuia uingizaji wa bidhaa chakavu za umeme (used) kutoka nje ya nchi ili kuhifadhi mazingira na kulinda afya za wananchi. 

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Bishara na Maendeleo ya Viwanda Mhe Dkt Salum Soud Hamed katika Mkutano na wafanyabiashara wa bidhaa chakavu za umeme wakati akitoa taarifa ya Serikali kwa bidhaa hizo ambazo zimetumika, katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Wilaya ya Mjini 

Amesema Serikali inatarajia kufungia bidhaa hizo baada ya kipindi cha miezi 12 ili kutoa muda kwa wafanyabiasha kuuza bidha zilipo na kupunguza hasara kwa jamii.

Naibu huyo amezitaja bidhaa zitakazofungiwa ni pamoja na komputa na friji ili kupunguza uharibifu wa mazingira na kulinda afya za wananchi.

"Kila biashara lazima iwekewe taratibu zake na hii biashara ya vitu chakavu vya umeme lazima nayo iwekewe taratibu zake" amesema Mhe Dkt Salum

Ameeleza kuwa bidhaa nyingi zinazoingizwa nchini hazifai na zinakuwa hatarishi kwa mtumiaji pia huchafua mazingira kwa ujumla pamoja na kusababisha maradhi mbalimbali jambo ambalo linarudisha nyumba maendeleo ya wananchi

Amesema kuwa kuwekwa kwa taratibu hizo si kumkandamiza mfanya biashara bali serikali inakusudi kumlinda mtumiaji na maslahi ya taifa kwa ujumla.

Nae Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Habiba Hassan Omar amesema Serikali imeamua kuweka utaratibu huo kwa kushirikiana na wafanyabiashara pamoja na wadau mbalimbali wa biashara na kuangalia athari ambazo zinazojitokeza kutokana na bidhaa hizo.

Aidha amefahamisha kuwa kutokana na changamoto hizo Serikali kwa kushirikiana na wadau wa bishara imekuwa na mpango wa kuzuia uingizaji wa bidhaa hizo kwa maslahi wa wananch na Taifa kwa ujumla.

Nao wafanyabiashara wameomba kuwekewa vikao ili kupata muda wa kutafakari hatua zinazoweza kufanyika ili kuepuka hasara katika biashara hiyo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo tarehe 30 Oktoba 2026, amekutan...
30/10/2026

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo tarehe 30 Oktoba 2026, amekutana na viongozi wa taasisi na makampuni mbalimbali ya Korea Kusini jijini Seoul, kujadili fursa za ufadhili, uwekezaji na utaalamu katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya maendeleo Zanzibar.

Katika mikutano hiyo na K-FINCO, HEERIM, Sejong Plant, SAMOO C.M. Architects & Engineers na Sung Shin Rolling Stock Technology Ltd. (SSRST), majadiliano yamejikita katika miradi ya bandari, usafiri wa baharini, barabara, miundombinu ya mijini, nishati, utalii na viwanda, pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Binguni na Kituo cha Kimataifa cha Mikutano na Maonesho Zanzibar (MICE).

Aidha, mazungumzo yamehusu uwezekano wa kushirikiana katika miradi ya maji safi na salama, usafishaji wa maji taka, uwekezaji katika uhifadhi wa mazao ya uvuvi kwa njia ya baridi na upatikanaji wa masoko ya kimataifa.

Sambamba na hayo, kampuni ya Sung Shin Rolling Stock Technology Ltd. imeonesha nia ya kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mpango wa kurejesha huduma ya reli ya abiria na utalii Zanzibar.

Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza kuendelezwa kwa mawasiliano ya kitaalamu ili kuweka mikakati ya utekelezaji na mifumo ya ufadhili wa miradi hiyo kwa kuzingatia taratibu za Serikali.

Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Riziki Pembe Juma amesema Wizara itaendelea kusimamia na kifatilia kwa ...
29/10/2026

Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Riziki Pembe Juma amesema Wizara itaendelea kusimamia na kifatilia kwa Karibu Ujenzi wa Uwanja wa Afcon Fumba kuhakikisha unakamilika kwa wakati

Ameyasema hayo huko Fumba Wilaya ya Magjaribi B' katika ziara kutembelea na kuangalia maendeleo yaliyofikiwa katika Ujenzi wa uwanja huo

Amesema kuwa kasi a Ujenzi wa maendeleo ya uwanja wa huo ni ya kuridhisha kwani kuna mabadiliko makubwa yanayoendelea

Aidha amefahamisha kuwa zaidi ya viti 2000 tayar vimeshawekwa katika uwanja huo hatua ambayo ni kubwa na ya kuridhisha

Dkt Riziki ameongeza kuwa maendeleo ya Ujenzi ya uwanja huo yanaendelea vizuri kwani tayari imeshafikia asilimia 87 ya uwanja wote na wanatarajiwa Hadi kufikia
imeshafikia ya Ujenzi wa uwanja Disemba 31 iwebtayari omeshakamilika

Akizungumzia kuhusu miundo mbinu katika eneo hilo amesema yanaendelea vizuri kwani yameshafikia asilimia 81 ya miundombin yote

Katika hatua nyengine Dkt Riziki amefahamisha kuwa ifikapo Novemba wanatarajiwa paa la uwanja huo litakua limekamika

Aidha mefahamisha kuwa kwa upande wa viwanja vya mazoezi navyo vinaendelea vizuri

Nae Mshauri Elekezi kutoka Kampuni ya Alhitmy Mhammed Noor amesema kuwa asilimia iliyofikiwa katika Ujenzi ni nzuri na wanaendelea kufanya jitihada kuhakikisha Mradi unakamilika kwa wakati

Aidha amesema kwa upande wa uwekaji wa viti na mazingira ya nje hadi kufikia Novemba wanategemea kufika asilimia 90

waandishi wa habari wametakiwa kuutangaza Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na usajili wa taarifa za Ardhi Nchi (LARIS) ili wa...
29/10/2026

waandishi wa habari wametakiwa kuutangaza Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na usajili wa taarifa za Ardhi Nchi (LARIS) ili wananchi waweze kupata uwelewa juu ya Mradi huo

Wito huo umetolewa na Afisa Mawasiliano na kujenga uwelewa wa Mradi Bi Jacqueline Jacob Laisser katika Ukumbi wa Ofisi ya LARIS Maisara katika mafunzo yaliyowashirikisha waandishi wa habari

Amesema waandishi wa habari ni kioo kwa jamii hivyo wana wajibu wa kutoa taarifa ya kutangaza Mradi huo ili jamii iweze kufahamu

Mratibu wa Mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Usajili wa Ardhi (LARIS) Zanzibar ambae pia ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo Ibrahim Khalid Mambo amesema Laris ni mfumo unaounganisha Usimamizi wa ardhi katika kupanga, kupima, kusajili na kutoa hati za utambuzi ambapo mfumo huo utasaidia katika kutatua migogoro

Mratibu huyo ameeleza kuwa Mradi huo umelenga kutengeneza mfumo wa Usimamizi wa ardhi ambao
utarahisisha utoaji wa taarifa za ardhi kwa haraka na usahihi kwa wananchi sambamba na kutambulisha eneo la mhusika

Amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kutoa uwelewa kwa waandishi wa habari kufahamu namna ya Mradi huo unavyotekelezwa

Ameongeza kuwa mfumo huo wa teknolojia ya kisasa ni jumuishi hivyo utasaidia kuonesha taarifa tofauti ikiwemo Umiliki sahihi, Upimaji, usajili na utambuzi wa ardhi

"Mfumo ni mmoja ambao utakaounganisha mifumo yote katika matumizi ya Ardhi", ameeleza Mratibu huyo

Naonwashirikibwaafunzo hayo wameishukuru Mradi wa LARIS kwa kuandaa mafunzo hayo na kuahidi kuyafanyia KAZI ili jamii ipate uwelewa

Mradi huo wa miezi 24 umenza Juni 2026, unatekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya makaazi kwa kushirikiana na Kampuni ya Ign fi kutoka Ufaransa.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amepokea bendera ya Jukwaa la Sera ...
29/10/2026

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amepokea bendera ya Jukwaa la Sera za Utalii kwa Visiwa (ITOP), ikiwa ni ishara rasmi ya Zanzibar kuwa mwenyeji wa Jukwaa la 28 la ITOP mwaka 2027.

Rais Dkt. Mwinyi amekabidhiwa bendera hiyo na Gavana wa Jeju, Mhe. Wi Seong-gon, leo tarehe 29 Oktoba 2026, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Jukwaa la 27 la ITOP iliyofanyika Jeju Stone Park, Kisiwa cha Jeju, Jamhuri ya Korea (Korea Kusini).

Uenyeji huo utaipa Zanzibar fursa ya kutangaza vivutio vyake vya utalii, utamaduni na uwekezaji, pamoja na kuimarisha ushirikiano na maeneo ya visiwa duniani katika kukuza utalii endelevu na maendeleo ya uchumi.

ITOP ina maeneo 12 wanachama ambayo ni Jeju, Bali, Hainan, Okinawa, Southern Province ya Sri Lanka, Hawai‘i, Zanzibar, Phuket, Cebu, Penang, Galápagos na South Aegean.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amependekeza kuanzishwa kwa ushirik...
29/10/2026

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amependekeza kuanzishwa kwa ushirikiano wa kindugu kati ya Zanzibar na Kisiwa cha Jeju, Jamhuri ya Korea (Korea Kusini), utakaolenga kuimarisha ushirikiano katika utalii endelevu, uchumi wa buluu, nishati mbadala, biashara na uwekezaji, pamoja na elimu na mafunzo.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 29 Oktoba 2026, alipokutana na Gavana wa Jeju, Mhe. Wi Seong-gon, kisiwani humo, akieleza kuwa Zanzibar inaweza kunufaika na uzoefu wa Jeju katika usimamizi wa utalii, matumizi ya nishati ya jua na upepo, uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya uchumi wa bahari.

Aidha, amewakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara wa Jeju kuangalia fursa za uwekezaji zilizopo Zanzibar, huku Gavana Wi Seong-gon akieleza utayari wa kuendeleza ushirikiano huo kupitia majadiliano ya kitaalamu na kuweka utaratibu wa kufuatilia hatua zinazofuata.

RAIS DKT. MWINYI KUELEKEA KOREA KUSINI KUSHIRIKI MAJUKWAA YA UTALIIRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi...
25/10/2026

RAIS DKT. MWINYI KUELEKEA KOREA KUSINI KUSHIRIKI MAJUKWAA YA UTALII

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, anatarajiwa kuondoka nchini leo, tarehe 25 Oktoba 2026, kuelekea Korea Kusini kushiriki Jukwaa la 27 la Sera za Utalii kwa Visiwa na kutembelea Maonesho ya Dunia ya Visiwa 2026, yatakayofanyika Jijini Yeosu, katika Kisiwa cha Jeju.

Ushiriki huo unalenga kuitangaza Zanzibar kimataifa, kuimarisha ushirikiano katika sekta ya utalii, kuvutia uwekezaji na kuongeza idadi ya watalii, hatua zitakazochangia kukuza uchumi na fursa za ajira kwa wananchi.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
24/10/2026

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Wakala wa Chakula, Dawa na vipodozi Zanzibar (ZFDA) imeteketeza jumla ya tani saba za bidhaa mbalimbali za chakula zisiz...
24/10/2026

Wakala wa Chakula, Dawa na vipodozi Zanzibar (ZFDA) imeteketeza jumla ya tani saba za bidhaa mbalimbali za chakula zisizofaa kwa matumizi ya binadamu katika jaa kuu la Kibele, ikiwa ni hatua ya kulinda afya za walaji.

Bidhaa zilizoteketezwa ni pamoja na tani nne za soda, tani moja ya tende na tani mbili za bidhaa mchanganyiko, zilizobainika kuharibika na hazifai kwa matumizi ya binadamu.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Afisa Uhusiano wa ZFDA, Fatuma Makame Juma, amesema baadhi ya bidhaa hizo zilipatikana kupitia ukaguzi, na nyingine zilisalimishwa na mfanyabiashara baada ya kubaini kuwa hazifai kwa matumizi.

Hivyo amewataka wafanyabiashara kutoa taarifa mapema na kuepuka kuuza bidhaa hatarishi ili kulinda usalama wa mtumiaji.

Naye mwakilishi wa kampuni ya Mosal, Freddy Robert, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wafanyabiashara na ZFDA katika kuondoa bidhaa zisizofaa sokoni na kulinda afya za walaji.

ZFDA ina jukumu la kusimamia usalama wa chakula, dawa na vipodozi Zanzibar, ikiwemo kufanya ukaguzi na kuchukua hatua dhidi ya bidhaa zinazoweza kuhatarisha afya ya jamii.

Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar- ZFDA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewaapisha wajumbe wa Tume ya Mipa...
22/10/2026

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewaapisha wajumbe wa Tume ya Mipango Zanzibar.

Tume hiyo ina jukumu la kuratibu mipango ya maendeleo, kuweka vipaumbele na kufuatilia utekelezaji wake.

Hafla ya uapisho imefanyika leo, tarehe 22 Oktoba 2026, Ikulu Zanzibar, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

Wajumbe walioapishwa ni:
1. Mhe. Mansura Mosi Kassim
2. Mhe. Dkt. Mwinyi Talib Haji
3. Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed
4. Mhe. Omar Said Shaaban
5. Mhe. Rahma Kassim Ali
6. Mhe. Shaaban Ali Othman
7. Mhe. Dkt. Juma Malik Akil
8. Mhe. Dkt. Nasra Nassor Omar
9. Mhe. Amina Khamis Shaaban
10. Mhe. Joseph J. Semboja
11. Mhe. Dkt. Twahir Mohammed Khalfan

Address

Rahaleo
Zanzibar

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 13:00

Telephone

+255777416213

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Idara ya Habari Maelezo Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Idara ya Habari Maelezo Zanzibar:

Shortcuts

Share

Nearby government services