Kampuni ya Meli Tanzania

Call Directions Website Contact the organization

Kampuni ya Meli Tanzania KAMPUNI YA MELI TANZANIA (TASHICO) ilijulikana k**a MSCL ilianzishwa rasmi tarehe 8/12/1997 baada ya kutenganishwa kutoka katika shirika la reli nchini(TRC).

TASHICO ni Kampuni ya Serikali inayosafirisha abiria na mizigo katika Maziwa Makuu.

01/11/2026

SEHEMU YA PILI HATUA ZA UJENZI MELI MPYA - KIGOMA

30/10/2026

HIVI NDIVYO MELI MPYA YA TASHICO INAVYOJEGWA KIGOMA.

18/10/2026

TASHICO YAIREJESHA MT UKEREWE ZIWA VICTORIA.
NI MELI YA MSAADA MKUBWA ZIWANI.

06/10/2026
30/09/2026

NI ZAIDI YA MELI.. VODACOM YAVINJARI TASHICO NA MV MEW MWANZA.

25/09/2026
*TANZANIA YAZIDI KUJENGA HADHI YAKE KIMATAIFA KATIKA SEKTA YA UCHUKUZI, YAPEWA UWENYEKITI MWENZA JUKWAA LA MAWAZIRI BEIJ...
23/09/2026

*TANZANIA YAZIDI KUJENGA HADHI YAKE KIMATAIFA KATIKA SEKTA YA UCHUKUZI, YAPEWA UWENYEKITI MWENZA JUKWAA LA MAWAZIRI BEIJING*

Tanzania imepewa nafasi ya Uwenyekiti Mwenza wa Jukwaa la Mawaziri wa Sekta ya Uchukuzi linalofanyika jijini Beijing, China ambapo Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, ameshiriki katika jukwaa hilo leo tarehe 22 Septemba 2026, akiongoza kwa pamoja na Waziri wa Uchukuzi wa China, Mhe. LIU Wei

Jukwaa hilo la siku tatu limewakutanisha zaidi ya Mawaziri 20 wa Uchukuzi kutoka nchi mbalimbali kwa ajili ya kujadili maendeleo ya sekta hiyo, kubadilishana uzoefu na kuimarisha miundombinu na huduma za usafirishaji, pia linahamasisha utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa China wa Global Development Initiative (GDI)

Akizungumza katika jukwaa hilo, Prof. Mbarawa amesema Tanzania imefanya uwekezaji mkubwa katika reli ya kisasa, barabara, bandari na viwanja vya ndege,amesema uwekezaji huo unalenga kurahisisha usafirishaji wa watu na mizigo, kuunganisha maeneo ya vijijini na mijini, kuchochea biashara na kuongeza fursa za kiuchumi

Aidha, Prof. Mbarawa ametumia fursa hiyo kuwaalika taasisi za serikali, wadau wa maendeleo na sekta binafsi kuwekeza Tanzania, akisisitiza kuwa Sekta ya Uchukuzi ina fursa mbalimbali za uwekezaji “Tanzania ina fursa nyingi kupitia Sekta ya Uchukuzi, hivyo ninawaalika taasisi za serikali, wadau wa maendeleo na sekta binafsi kuwekeza katika Sekta ya Uchukuzi Tanzania,” amesema

Ushiriki wa Tanzania katika jukwaa hilo unaipa fursa ya kushirikisha uzoefu wake, kujifunza teknolojia na mbinu kutoka nchi nyingine, pamoja na kutafuta fursa za uwekezaji katika miradi ya uchukuzi

Tanzania na China zina historia ya muda mrefu ya ushirikiano katika Sekta ya Uchukuzi, ikiwemo reli ya TAZARA na usafiri wa majini kupitia SINOTASHIP, Nafasi ya Uwenyekiti Mwenza inaongeza fursa za kuendeleza ushirikiano huo katika miundombinu, teknolojia na uwekezaji.

CCM KIGOMA YARIDHISHWA NA UKARABATI WA MV LIEMBA - KUTARAJIA KUANZA SAFARI OKTOBAKamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi ...
21/09/2026

CCM KIGOMA YARIDHISHWA NA UKARABATI WA MV LIEMBA - KUTARAJIA KUANZA SAFARI OKTOBA

Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma imeridhishwa na hatua ya ukamilishaji wa ukarabati wa Meli ya MV Liemba inayotarajiwa kuanza kutoa huduma zake za usafiri hivi karibuni Ziwa Tanganyika.

Kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Ndg. Jamal Abdalah Tamim, akiambatana na wajumbe wake, ilifanya ziara katika mradi huo uliopo Bandari ya Kigoma kwa kukagua maeneo yote ya ndani na nje ya meli hiyo.

Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Mwenyekiti Tamim alisema:

"Tumeridhidhishwa na hatua iliyofikiwa kwa sasa ya ukarabati wa meli hii.Kinachosubiriwa kwa sasa ni kukamilisha taratibu ndogo ndogo za kiutawala ili safari zianze''

Kwa mujibu wa wataalamu, ukarabati wa MV Liemba umekamilika kwa asilimia 99, ambapo kwa sasa kinachosubiriwa ni kukamilika kwa taratibu za ndani za ukaguzi na upatikanaji wa vibali ili meli hiyo ianze safari zake rasmi mapema mwanzoni mwa mwezi Oktoba 2026.

Address

Tanzania Shipping Company Ltd
Mwanza
33000

Opening Hours

Monday 07:30 - 17:30
Tuesday 07:30 - 17:30
Wednesday 07:30 - 17:30
Thursday 07:30 - 17:30
Friday 07:30 - 17:30
Saturday 07:30 - 17:30
Sunday 07:30 - 17:30

Telephone

+255739606600

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kampuni ya Meli Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Kampuni ya Meli Tanzania:

Shortcuts

Share