Bank of Tanzania

Directions Website Contact the organization

Bank of Tanzania This is the official page of the Bank of Tanzania

13/11/2026
BoT YAWATAKA WAFANYABIASHARA KUONGEZA MATUMIZI YA MIFUMO YA MALIPO YA KIDIJITALIBenki Kuu ya Tanzania (BoT) imewataka wa...
11/11/2026

BoT YAWATAKA WAFANYABIASHARA KUONGEZA MATUMIZI YA MIFUMO YA MALIPO YA KIDIJITALI

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewataka wafanyabiashara wa Kariakoo kutumia mifumo ya malipo ya kidijitali katika shughuli zao za biashara ili kuongeza usalama wa miamala, kurahisisha upokeaji wa malipo na kuongeza ufanisi wa biashara zao.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa wa Benki Kuu ya Tanzania, Bi. Lucy Shaidi, wakati akifungua mkutano wa uelimishaji kuhusu mifumo ya malipo uliohusisha viongozi na wafanyabiashara wa Kariakoo, uliofanyika katika Ofisi za Benki Kuu, Makao Makuu Ndogo ya Dar es Salaam, Novemba 11, 2026.

Amesema mkutano huo umeandaliwa kwa lengo la kuwajengea wafanyabiashara uelewa kuhusu mifumo mbalimbali ya malipo, matumizi yake salama na faida zake katika shughuli za kila siku za biashara.

Aidha, mkutano huo umeiwezesha Benki Kuu kupata fursa ya kusikiliza maoni na changamoto zinazowakabili wafanyabiashara katika matumizi ya mifumo hiyo inayojumuisha malipo kwa kutumia kadi za benki na mashine za POS, simu za kiganjani, benki mtandao, Lipa Namba, msimbomilia (TANQR), hundi pamoja na uhamishaji wa fedha kutoka benki moja kwenda nyingine.

Akitoa wasilisho kuhusu faida za mifumo ya malipo ya kidijitali, Meneja Msaidizi kutoka Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo ya Taifa ya Benki Kuu, Bw. Fabian Kasole, amesema mifumo hiyo inawezesha kuongeza usalama wa fedha kwa kupunguza hatari ya wizi na matumizi ya noti bandia, kutunza kumbukumbu za miamala, kurahisisha upatikanaji wa mikopo kupitia kumbukumbu za biashara, pamoja na kuongeza kasi na urahisi wa kupokea malipo.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wa Kariakoo, Kaimu Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo, Bw. Donald Kibuna, amesema matumizi ya mifumo ya malipo ya kidijitali yamewasaidia kuokoa muda na kurahisisha miamala ya fedha kwa kuwawezesha kufanya malipo papo hapo bila kulazimika kwenda benki.

Amesema hali hiyo imewawezesha kuendelea na shughuli zao za biashara kwa ufanisi zaidi. Aidha, wafanyabiashara hao wameishukuru Benki Kuu kwa kuandaa mkutano huo na kupongeza juhudi zake katika kuimarisha huduma za malipo nchini.

Uhamasishaji wa matumizi ya malipo ya kidijitali ni sehemu ya juhudi za Benki Kuu katika kuunga mkono utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayolenga kujenga uchumi imara, wa kisasa na wa kipato cha juu, ambapo teknolojia na uchumi wa kidijitali ni miongoni mwa nguzo muhimu za maendeleo.

Benki Kuu itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali, wakiwemo wafanyabiashara, kusikiliza maoni yao na kufanyia kazi changamoto zinazojitokeza katika matumizi ya mifumo ya malipo ili kuimarisha mazingira ya kufanya biashara kwa usalama, urahisi na ufanisi zaidi.

09/11/2026
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kushirikiana na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), wamezindua Programu...
09/11/2026

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kushirikiana na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), wamezindua Programu Maalum ya Elimu ya Fedha kwa wanafunzi wa elimu ya juu wanaonufaika na mikopo ya HESLB, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha vijana kuwa na maarifa na stadi za kusimamia fedha binafsi.

Akizungumza katika hafla iliyofanyika katika ofisi za BoT jijini Dar es Salaam, Novemba 9, 2026, Gavana wa BoT, Bw. Emmanuel Tutuba alisema programu hiyo ni hatua muhimu katika kuwaandaa vijana kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya uchumi wa nchi, hususan katika kufanikisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayolenga kujenga uchumi imara, jumuishi na shindani.

Alisisitiza kuwa elimu ya fedha ni muhimu kwa kila Mtanzania, wakiwemo wanafunzi, wazazi, walezi na wadau wengine, ili kuwawezesha kupanga na kusimamia mapato na matumizi yao kwa kuzingatia vipaumbele.

Alieleza kuwa programu hiyo itatekelezwa kupitia mfumo wa akaunti binafsi ya mwanafunzi unaojulikana k**a Students’ Individual Permanent Account (SIPA), ambapo maudhui ya elimu ya fedha yaliyoandaliwa na BoT yatawekwa ili kuwawezesha wanafunzi kuyapata kwa urahisi.

Aliongeza kuwa maudhui hayo pia yameandaliwa katika mfumo wa kitabu kitakachopatikana kwa umma kupitia tovuti ya BoT, hatua inayopanua wigo wa upatikanaji wa elimu hiyo hata kwa wanafunzi ambao si wanufaika wa mikopo ya HESLB.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dkt. Bill Kiwia, alisema jukumu la Bodi hiyo haliishii katika kutoa mikopo na ufadhili kwa wanafunzi wenye sifa na mahitaji, bali pia kuwawezesha wanufaika kuwa na uelewa wa matumizi, usimamizi na urejeshaji wa mikopo.

Alieleza kuwa elimu hiyo itawasaidia wanafunzi kuelewa umuhimu wa kutumia huduma rasmi za kifedha, kuweka akiba na kutimiza wajibu wa kurejesha mikopo kwa wakati ili kuimarisha mnyororo wa upatikanaji wa mikopo kwa vizazi vijavyo.

Programu hiyo inaunga mkono juhudi za Serikali pamoja na Mpango wa Tatu wa Taifa wa Ujumuishi wa Kifedha (NFIF 2023-2028), unaotambua vijana kuwa miongoni mwa makundi muhimu yanayopaswa kunufaika na elimu ya fedha.

BoT INAUPIGA MWINGI MASHINDANO YA SHIMMUTA Benki Kuu ya Tanzania (BoT), inaonesha kiwango cha hali ya juu katika Mashind...
07/11/2026

BoT INAUPIGA MWINGI MASHINDANO YA SHIMMUTA

Benki Kuu ya Tanzania (BoT), inaonesha kiwango cha hali ya juu katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA), yanayoendelea mkoani Morogoro.

BoT inashiriki mashindano hayo kupitia timu zake za michezo mbalimbali, zikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa kikapu, mpira wa wavu pamoja na riadha.

Katika mchezo wa mpira wa pete, BoT imeanza vyema kwa kuichapa timu ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) magoli 20 kwa 18 katika mchezo wake wa kwanza.

Aidha, katika mchezo wa pili uliofanyika leo, Novemba 7, 2026, timu ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) iliponea chupuchupu kugaragazwa na BoT ambapo ililazimisha sare ya magoli 23 kwa 23.

Vilevile, timu ya mpira wa miguu ya BoT imepata ushindi mnono wa mabao 4 kwa 1 dhidi ya timu ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) katika mchezo uliofanyika leo Novemba 7 2026. Ushindi huo unaifanya timu ya mpira wa miguu ya BoT kuwa miongoni mwa timu tishio katika mashindano hayo.

Ushiriki wa BoT katika mashindano ya SHIMMUTA ni kilelezo cha jitahada za Benki Kuu katika kuimarisha afya na kujenga ushirikiano mzuri baina ya watumishi kutoka taasisi mbalimbali za Serikali hatua inayosaidia kustawisha maelewano na kubadilishana uzoefu ili kutekeleza majukumu ya Serikali kwa ufanisi.

Mashindano hayo yenye kauli mbiu ya ‘Michezo ituunganishe Kuelekea AFCON 2027’ yalianza tarehe 6 Novemba na yanatarajia kuhitimishwa tarehe 21 Novemba 2026.

Address

16 Jakaya Kikwete Road
Dodoma
40184

Opening Hours

Monday 08:30 - 12:30
14:30 - 16:30
Tuesday 08:30 - 12:30
14:30 - 16:30
Wednesday 08:30 - 12:30
14:30 - 16:30
Thursday 08:30 - 12:30
14:30 - 16:30
Friday 08:30 - 12:30
14:30 - 16:30

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Bank of Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Bank of Tanzania:

Shortcuts

Share